Besta Ft Dully Sykes - Kama Ulivyo (Audio) | REWIND

MOJA ya wasanii wa kike waliotamba katika game ya Bongo Flava Tanzania usipomtaja Besta basi hauijui Bongo vizuri. Besta Prosper ni mwanadada aliyefanya vizuri kwenye game ya bongo na hits songs kama Kati yetu, Kama Ulivyo na Baby Boy. Besta mtoto wa kihaya aliyemaliza elimu yake ya sekondari katika shule ya msalato iliyopo mkoani morogoro na baada ya hapo St. Mary's ambapo alimaliza kidato cha sita na hivi sasa amehitimu Nkumba University nchini Uganda ambapo amechukua shahada ya Business and Information Technology (IT), unaweza kumweka msanii huyu katika list ya wasanii wasomi hapa nchini. Besta Yuko Wapi? Kwa sasa bidada huyo anaishi na msanii mwenzake Marlaw, Kwenye interviews nyingi amekuwa akisema kuwa amekuwa busy na majukumu ya kifamilia ila atarudi tena kuwakilisha Bongo Flava. Kama Ulivyo ni moja ya Audio alizowahi kuzitoa na hii alimshirikisha Dully Sykes. Ukisikiliza vocals na melody ya mdundo ni mziki flani hivi mzuri. Tuskilize pamoja kisha usisahau kucomment.DOWNLOAD AUDIO

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post