Diamond Platnumz Aachiwa Kwa Dhamana

Kamanda wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa amesema msanii Naseeb Abdul maarufu Diamond Platinumz jana Jumatatu Aprili 16 alishikiliwa na polisi kwa ajili ya mahojiano kufuatia kusambaza picha zisizo na maadili.


Mambosasa amesema  kuwa Diamond alihojiwa na kupewa dhamana jana Jumatatu huku uchunguzi zaidi ukiwa unaendelea na utakapokamilika ataitwa tena polisi.


“Alihojiwa jana na akapewa dhamana, upelelezi unaendelea,” amesema Mambosasa.


Leo katika kipindi cha maswali na majibu bungeni, Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk Harrison Mwakyembe amesema polisi inamshikilia msanii huyo na Nandy ambao kwa nyakati tofauti wanadaiwa kusambaza picha sisizo na maadili kwenye mtandao.


Wasanii hao wanadaiwa kusambaza picha hizo kupitia mtandao wa kijamii wa Instagram.

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post