Walter Chilambo Kupewa Support na Paul Makonda

Msanii wa nyimbo za Injili nchini Walter Chilambo ambaye sasa anafanya vyema na wimbo wake mpya 'Only You' amepewa nguvu na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda, Erick Shigongo pamoja na msanii Jux katika kuhakikisha wimbo wake huo unawafikia watu.

Kutokana na ujumbe ambao upo ndani ya wimbo huo na uzuri wake pia umemlazimu Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe, Paul Makonda mara kadhaa kuutumia wimbo huo kwenye mitandao yake ya kijamii bila kusema neno lolote lile zaidi ya kufikisha ujumbe wake kwa watu kupitia ujumbe ambao upo ndani ya wimbo huo kuwa anamtegemea Mungu tu na si kitu kingine katika maisha yake.

Aidha Mhamasishaji na Mkufunzi wa Ujasiriamali Afrika Mashariki na Kati, Eric Shigongo pia ameuzungumzia wimbo huo na msanii huyo na kusema ni kati ya wasanii wazuri sana kwenye injili japo hawapewi nguvu kutokana na kutokuwa na mbwembwe katika kazi zao.

"Mara nyingi nimeshaambiwa huyu mtoto ni tishio katika Gospel, sema unyenyekevu wake ndio unamfanya asionekane mapema, hebu sikiliza huu wimbo halafu uniambie mwenyewe" Shigongo

Kwa upande wake Jux alichukua baadhi ya maneno ya wimbo huo ishara kuonyesha kwamba amevutiwa na kazi hiyo mpya wa Walter Chilambo.

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post