Jokate Mwegelo Afunguka Kuhusu Tuzo za Sinema Zetu

Jokate Mwegelo Afunguka Kuhusu Tuzo za Sinema Zetu "Mapungufu ni Sehemu ya Kujifunza"

Jokate Afunguka

Kama Mlezi wa Tuzo Hizi #Sziff2019 Nawapongeza Sana @azamtvtz @sinemazetu103 kwa kufanikisha Tuzo kwa mara ya pili mwaka huu 2019. Zaidi kwa namna ambavyo mnasadia kuibua vipaji vipya na kuvifanya vionekane na kutambulika na kupewa heshima ndani na nje ya nchi. Mnachangamsha Tasnia Nzima Ya Filamu Nchini na Sasa Tunaona Ushindani Mkubwa ambao naamini utakuwa ni kichocheo cha maendeleo na ubora kwenye tasnia hii. Mnaongeza kiu ya kutaka mafanikio makubwa zaidi ya hapa tulipo. Na mapungufu yaliyojitokeza ni sehemu ya kujifunza. Nina imani mwakani tutafanya vizuri zaidi na kukonga zaidi nyoyo za mashabiki.
.
.
Niwapongeze wote walioshiriki na walioshinda Tuzo. Lakini pia niwakumbushe hakuna Tuzo Kubwa kama ya mapenzi makubwa kutoka kwa mashabiki. Tuzo hii haishindaniwi. Ni baraka za Mwenyezi Mungu. Kwa hivyo nyote ni washindi.
Zaidi nimefurahi kuona kaka yangu @adamjumanxl na team yake nzima wakishinda Tuzo 5. Adam Juma ni mtu ambaye ana passion kubwa sana na tasnia yetu ya filamu tangia enzi zake za ku-shoot music videos. Lakini pia kaka yangu John Kallaghe the genius kwenye directing na dada yangu @esieesther na my brother Azmil Shivji. Weledi wenu na kiu yenu nyuma ya pazia imeonekana na leo tunafurahia ushindi wenu.
.
.
Na kwa wadogo zetu Flora na Rashid aka #KAMWENE mmeshinda Tuzo Kubwa za Usiku Huo. You are STARS Now!!! Ninyi ni NYOTA!! Ona Kamwene ilivyo-hit.
Hiyo ndio nguvu ya Sanaa!! Nilifurahii zaidi kwenye hotuba zenu za kupokea tuzo mlivyoongelea AMANI na kuenzi LUGHA Yetu!! Mmeonyesha ukomavu licha ya umri wenu mdogo. Kongole!!!!
.
.
Kwa the ICONS wa Filamu nchini tuendelee kupendana na ku-support juhudi zote zinazoelekea kwenye kukuza vipaji na tasnia yetu. We love you and we thank you for what you have done and continue to do for this industry ๐Ÿ™Œ๐Ÿ™Œ
Previous Post Next Post