Mwanafunzi Ajiua kwa Kijipiga Risasi Kichwani

Mtu  mmoja aliyetambulika  kwa jina la Jasmini Ngoye (18), mwanafunzi wa kidato cha nne shule ya sekondari Lupanga iliyopo manispaa ya Morogoro,  amekutwa amukufa baada ya kujipiga risasi ya kicha huku chanzo cha kifo hicho kikidaiwa kuwa ni msongo wa mawazo. .
 

Tukio hilo limetokea Jumanne Februari 19, 2019 eneo la Kola B mtaa wa Bogwa na mwili wa mwanafunzi huyo ulikutwa ukiwa na bastola pembeni aina ya Bereta ikiwa na magazini moja na ganda la risasi.
 

Akizungumzia tukio hilo leo Alhamisi Februari 21, 2019 Kamanda wa Polisi mkoa wa Morogoro, Wilbroad Mutafungwa amesema muda mfupi baada ya tukio hilo, shemeji wa binti huyo, Profesa Hamisi Mahigi alijitokeza na kueleza kuwa bastola hiyo ni yake na anaimiliki kihalali.
 

Kamanda huyo amesema binti huyo aliacha ujumbe aliouandika katika kitabu chake cha kumbukumbu kabla ya kujipiga risasi, alimkabidhi rafiki yake aliyekuwa akisoma naye darasa moja, Imelda Milanzi.
 

Katika kitabu hicho mwandishi huyo ameandika; “Ni mtoto asiye na wazazi wake na asiyejua kazaliwa wapi? Mtoto huyu anatamani kukiona kifo chake wakati wowote, mtu yeyote atakayesoma dayari (diary) hii ndiye atakayeandika siku ya kifo chake.”
Amesema profesa huyo anashikiliwa na polisi kwa mahojiano. Mwili umehifadhiwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Morogoro.
This is Bongo Exclusive Official Website (Everything Exclusive) you can follow our social network pages or email us: bongoexclusive@hotmail.com

Become Our VIP Subscriber, Jiunge Sasa!

 
Top