Nimemkataza Mke Wangu Kujibusti Kabla ya Kupanda Jukwaani- Uchebe

Nimemkataza Mke Wangu Kujibusti Kabla ya Kupanda Jukwaani- Uchebe

Imebainika kuwa msanii Shilole amekatazwa kunywa pombe na mume wake, Uchebe hasa pale anapoenda kwenye matamasha yake ya muziki.

Akizungumza na kipindi cha Leo Tena cha Clouds FM, Uchebe amesema ilikuwa kawaida kwa Shilole kunywa pombe akipanda jukwaani ila kwa sasa amepunguza.

Nimemwambia usitumie kilaji kabla ya kupanda kwenye steji, anasema asipokunywa anawaona
watu sio wengi, nashukuru Mungu inafika hatua hafanyi hivyo hanywi pombe, kama kunywa basi
kidogo, amesema Uchebe.

Kwa sasa Shilole anafanya vizuri na wimbo wake mpya unakwenda kwa jina la Unanitekenya ambao amemshirikisha muimbaji Aslay, hii ni baada ya kutamba na wimbo Mchakamchaka
Previous Post Next Post