Watumishi 9 Wafariki kwa Ajali Morogoro

Watumishi 9 Wafariki kwa Ajali Morogoro

Watumishi tisa wa Halmashauri ya Ifakara wamefariki baada ya gari aina ya Land Cruiser walilokuwa wakisafiria kumshinda dereva na kutumbukia mtoni Wilayani Kilombero Mkoani Morogoro.

Kamanda wa Polisi mkoa wa Morogoro Wilbrod Mutafungwa amethibitisha kutokea kwa ajali ambapo amesema; Jana Saa 11 jioni katika Wilaya ya Kilombero gari lenye namba za usajili 994 Toyota Land Cruiser mali ya TAWA, gari ilikuwa inaenda Ifakara ilipofika daraja la Mto Kikwawila liliingia kwenye hilo daraja na kutumbukia Mtoni upande wa kushoto.

Watu tisa wamefariki; wa kwanza ni Salome Lucas, Shaban Yusuph, Glory Steven, Ludaya Mwakalebela, Silvester Mwakalebela, Maria Buginja, Sheila Shitambuni, Hassan Kayunga, Msafiri Kerald, hawa ni Watumishi wa Halmashauri ya Mji wa Ifakara Amesema RPC Morogoro.Previous Post Next Post