Mtangazaji Wa Clouds FM Ephraim Kibonde afariki dunia

Mtangazaji Wa Clouds FM Ephraim Kibonde afariki dunia

Mtangazaji wa Clouds FM Ephraim Samson Kibonde, amefariki dunia Alfajiri ya leo Machi 7, 2019 akiwa mkoani Mwanza.

Taarifa zilizotolewa na Meneja wa Maudhui wa Clouds Media Group, Sebastian Maganga, zinasema kwamba wanasubiri taarifa kutoka kwa Mganga Mkuu wa Mkoa wa Mwanza ili kuweza kupata taarifa zaidi juu ya kifo cha mtangazaji Ephraim Kibonde.
Ephraim Kibonde alianza kuugua akiwa mkoani Kagera, ambako walienda kwenye mazishi ya Mkurugenzi wa Vipindi na Uzalishaji, Ruge Mutahaba na baadaye kukimbizwa mkoani Mwanza.
Previous Post Next Post