Ommy Dimpoz afunguka kuhusu kufunga ndoa

Ommy Dimpoz afunguka kuhusu kufunga ndoa

Msanii wa muziki wa kizazi kipya Omary Nyembo Ommy Dimpoz amefunguka kuhusu suala la kuwa na mtoto pamoja na kufunga ndoa, ambapo amesema kuwa analifikiria bado.
Akizungumzia hilo Ommy Dimpoz amesema kuwa anatamani kuwa na familia lakini sio suala la kukurupuka kwakuwa, anahitaji kujipanga.

Kuhusu suala la kuingia kwenye majukumu mazito, yanahitaji muda wa kujipanga sio ufanye tu kwakuwa watu wanasema hivi kuhusu wewe, acha waseme lakini maneno yao yasifanye ukurupuke, amesema Ommy.

Hivi karibuni msanii huyo alipitia kipindi kigumu cha maradhi na kitu ambacho amekiri kuwa kimempa fundisho kubwa juu ya maisha ya binadamu kuwa si kitu hapa duniani.
Previous Post Next Post