Bifu la Q Chilla na TID laibuka Upya

Bifu la Q Chilla na TID laibuka Upya

Baada ya kutambulisha video ya wimbo wake mpya Tikisa, Msanii wa bongo fleva  Q Chief ameongea kuhusu kukosekana kwenye video mpya ya wimbo wa  TID, 'Najidai' wimbo ambao umetoka hivi karibuni ambayo Q Chila ameshirikishwa katia audio yake.
Akiongea na eNewz Q Chilla amesema ana sababu nyingi ambazo zimempelekea yeye kutokuwepo katika video hiyo lakini kubwa zadi ni kutokana na kauli na njia ambazo T.I.D alizitumia kumfikia Q Chilla na mwisho wa siku akaona hakuna sababu yeyote ya kutokea katika video hiyo kwa kuwa alionyesha kama kumdharau Q Chilla.

Ni kweli mimi na T.I.D tuna migogoro takribani miaka miwili sasa, nisingependa kuyaongelea sana madhambi ya mwenzangu lakini hata mimi nina mashabiki ambao wananifatilia na wanaona kila kitu kinachoendelea kwenye maisha yangu na nafikiri kwa watu wenye akili timamu wamefatilia na kugundua nani mwenye matatizo kati yetu, amesema Q Chilla.

Pamoja Q chilla kukosekana katika video pia amesikitishwa na namna ambavyo video hiyo ya Mnyama ilivyorekodiwa kwani haina kiwango wala hadhi kuwa video ya T.I.D kwa kuwa inaonekana ka video ambayo imerikodiwa na simu ya mkononi.
Previous Post Next Post