Manchester United kuikabili Barcelona LeoKocha wa Manchester United, Ole Gunnar Solskjaer anaamini timu yake inaweza kupata matokeo mbele ya Barcelona kwenye mchezo wa marudiano wa Champions League hatua ya robo fainali hii leo.

Kwenye mechi ya awali iliyochezwa Uingereza, Barcelona iliibuka na ushindi wa bao 1 – 0 kwenye uwanja wa Old Trafford na hivyo kuufanya mchezo wa leo kuwa mgumu hasa kwa United lakini, Solskjaer anaamini anao mpango wa kumdhibiti mchezaji hari duniani Lionel Messi pamoja wenzake.

“Tunafahamu kama tutakuwa kwenye ubora tutaweza kuwachanganya Barcelona, kwasababu tuliweza kufanya hivyo hapo awali pia,” amesema
kocha wa Manchester United, Ole Gunnar Solskjaer.

“Ndio mwishoni waliweza kuutawala mchezo, wakiwa na ‘possession’ lakini ukweli hawakuweza kuwa na madhara kwetu.”

“Nilipumzika wachache hapa kuwa tayari kwa Jumanne, lakini tuna mpango mzuri, natumaini. Natumaini ni nzuri. Ni mpango wowote. “

“Baadhi yao niliwapumzisha ili kuwa tayari kwaajili ya Jumanne, lakini tunampango na natumaini ni mzuri.”
Previous Post Next Post