Wema Sepetu Atoa ya Moyoni Jinsi 'Marafiki Wabaya Walinifelisha

Wema Sepetu Atoa ya Moyoni Jinsi 'Marafiki Wabaya Walinifelisha

Muigizaji Wema Sepetu ametoa somo kwa waigizaji na wadau waliopo kwenye tasnia ya filamu kupitia ushuhuda alioutoa wakati akizungumza kwenye kongamano la waigizaji lililoandaliwa na Bodi ya Filamu kwa kushirikiana na Chama cha Waigizaji Taifa , jana Jijini Dar es Salaam.

Wema amekiri kuwa moja ya vitu vilivyomrudisha nyuma nikushindwa kulinda brand(Chapa) yake, hivyo kujikuta akitumia muda mwingi mahakamani kutokana na kesi zinazomkabili.

Nili feli kwenye namna ya kulinda brand yangu na niliona hasara zake kubwa sana, hasara ilikuwa kubwa kuliko profit, kwanza nilipoteza muda mrefi sana nikiwa naaangaika na maswala ya polisi nikiwa mahakamani , nyote mlikuwa mkiona nikiwa naenda mahakani na mpaka dakika hii bado nina kesi ipo mahakamani sijui hatma yake‘’ Amesema Wema

Aidha, Wema ameongeza kuwa marafiki wabaya walichangia kumfanya apite njia sisizo sahihi na kupelekea kuingia matatizoni mara kwa mara. ‘’Kitu chakwanza ambacho mimi kilinifelisha kwenye kulinda brand yangu ni wrong Company (Marafiki wabaya) , leo hii mimi nimesimama hapa nikama nafanya testimony (Natoa ushuhuda), ukiwa unajihusisha na watu wasio sahihi huwezi kuendelea hata siku moja’’ ameongeza Wema Sepetu Wema amekuwa akikumbana na mkono wa sheria kutokana mtindo wa maisha yake, ikiwemo kufungiwa na bodi ya filamu kwa miezi sita kutojihusisha na shughuli za sanaa baada ya kusambaza picha za utupu.

Previous Post Next Post