Mangwair "a.k.a mimi" -The Album, Produced by P.Funk [Bongo Record].

 Mangwair "a.k.a mimi" -The Album, Produced by P.Funk [Bongo Record].

"a.k.a mimi" - Name of the Album, Produced by P.Funk {Bongo Record}.

1. MIKASI
➡️ft Mchizi Mox, P.Funk, Rah P, Mkoloni & Ferous
 

➡️ Nyimbo ambayo inaelezea maisha ya ujana/vijana unapofika muda wa jioni. Wengi wao hukutana na kupiga mahesabu ya kwenda kufanya starehe Clubs na sehemu nyngn kwa kuchangishana. Pamoja na hayo dhamira kuu inakuwa ni kwenda kutafuta wanawake hali ya kuwa wanawake wenyewe wanakuwa wanajiuza.
➡️ Mashairi katika nyimbo hii yamewekwa katika mpangilio wa vina wenye mtiririko mzuri na unaovutia zaidi bila kuharibu kile wanachokieleza kwa kupokezana.

2. BADO NIMO
➡️ featuring T.I.D (before Mnyama)
➡️Hi ndio nyimbo ambayo jina la album limesikika saana "A.K.A MIMI" kiasi kwamba wengine wanaiita hii nyimbo a.k.a mimi.
 

➡️Mashairi yamepangwa katika mtiriko mzuri kwa kuzzingatia vina bila kupoteza ujumbe uliokusudiwa. Katika wimbo huu Ngwair amejikita zaidi kuelezea kuhusu ugonjwa wa ukumu. Amesimama kama yeye ndio UKIMWI wenyewe ambapo ametaja majina tofauti tofauti ambayo yanajulikana lakin pia ameelezea namna gani Ukimwi unaambukizwa na ameeleza upo kwa wengi huku akiondoa dhana ya kuwa viongozi wa dini hawawezi pata ukimwi.
➡️ Pia, ameeleza namna gani huu ugonjwa umekosa dawa japokuwa watu wngn wanaaminisha kuwa zipo dawa.

3. ZAWADI
➡️Hii ni nyimbo nyingine ambayo Ngwair ameongelea suala zima la ugonjwa wa UKIMWI. Tofauti na "Bado nimo", humu Ngwair kaeleza zaidi namna gani wanawake wanashawishika kwa vitu vidogo vidogo ambavyo ndio tunasema Zawadi huku akielezea namna gani alikutana na binti akawa na mahusiano nae na mwishoe kumuambukia UKIMWI
➡️ Katika nyimbo hii unamsikia Ngwair akimuoffer bint ataje zawadi yeyote aitakayo huku bint akimjibu ya kuwa Zawadi ya HIV tayar imemtosha.
➡️ Kati ya nyimbo mzuri saaana yenye maelezo ya jinsi Ngwair anavyomhesabia bint zawadi alizompatia

4. DAKIKA MOJA
 

➡️Featuring Noorah (Baba Styles)
➡️ Hii nyimbo inaelezea kijana alivyokutana na bint katika moja ya kumbi za starehe na kuvutiwa nae huku akimuomba japo dakika moja ya kuweza kuongea nae, ndipo jina la nyimbo linapopatikana.
➡️ Hii ni moja ya nyimbo ambayo vijana wengi wa wakati nyimbo inatoka walitumia saana mashairi ya huu wimbo kutongozea wanawake kwani ilikuwa na maneno ya kusifia na kulainisha zaidi.

5. GHETO LANGU
➡️Achana na Ghetto ya Akon, hii ni tofauti kidogo. Ni nyimbo iliyojawa na majisifu kuhusu chumba (gheto). Katika nyimbo hii Ngwair amesifia saana chumba chake huku akiorodhesha vitu mbalimbali ambavyo vipo ktk gheto lake la Dodoma na lile la Kijitonyama.
➡️ Ngwair ameenda mbali kwa kuelezea namna marafiki zake wamekuwa wakienda hapo gheto kwake na wanawake zao lakin mwisho wa siku wanawake wanafall in love na Ngwair sababu ya Gheto

.... Kwa leo ngoja niishie hapo ila kwa wengine wanaweza endelea kuchambua;
 

6. Mademu Wangu
 

7. She got a Gwan
 

8. Weekend
 

9. Pokea simu
 

10. Sikiliza

Written By Hamza Athumani Mkata
Hamza Athumani Mkata
Previous Post Next Post