Pharrell Williams Anunua Mjengo Wenye Thamani Ya Tsh. Bilioni 69

Pharrell Williams

Kipindi hichi ambacho wengi tunakaa majumbani kuepukana na maambukizi ya Corona, Pharrell Williams ametafuta mahali pazuri zaidi.

Pharrell Williams

Mwimbaji huyo maarufu na mtayarishaji ameripotiwa kununua jumba la kifahari kwa ($30M) sawa na Bilioni 69 za Kitanzania. 

Pharrell Williams

Jumba hilo ambalo lipo mjini Miami Florida lilikuwa likimilikiwa na Mkurugenzi wa Univision, Ray Rodriguez na mkewe.

Pharrell Williams

Mjengo huo ulikuwa ukiuzwa kwa ($45M) kipindi cha mwaka mmoja na nusu uliopita lakini Pharrell kaupata kwa punguzo la asilimia 33. 

Pharrell Williams

Ndani ya jumba hilo lililotengenezwa na Cesar Molina kuna maajabu yake; Vyumba 9 vya kulala, Mabafu 11 nyumba nzima na ya wageni ambayo ipo kando. 

Pharrell Williams

Vingine ni gereji ya kuhifadhi magari hadi matano, jiko la ndani na nje, bwawa la kuogelea na makorombwezo mengine kibao.
Previous Post Next Post