Msanii wa muziki wa hip hop Bongo, Mwana FA amesema kolabo ya Diamond na kundi la Morgan Heritage ni kitu kilichomvutia kwani amekuwa shabiki wa kundi hilo kwa zaidi ya miaka 10 sasa. Rapper huyo ambaye kwa sasa anafanya vizuri na ngoma ‘Upo Hapo?’, amekiambia kipindi cha Uhondo cha E Fm kuwa kusikia kolabo hiyo kumeongeza mapenzi yake ya kimuziki kwa kundi hilo.
“Morgan Heritage ni miongoni mwa watu niliwasikiliza sana kwa miaka mingi, kama 2005/2006, nawasikiliza mpaka leo kama miaka 10, nawajua mpaka kwa majina ile familia” amesema Mwana FA. “Kwa hiyo niliposikia wamefanya na Mbongo ilinivutia na niliposikiliza ngoma ni nzuri, ipo tofauti kabisa hata Diamond siyo yule ambaye tumemzoea, kwa hiyo ngoma kali. Mimi love yangu kwa Morgan Heritage naona wameichukua moja kwa moja kwenye huu wimbo” ameongeza.
Morgan Heritage ni kundi linalofanya muziki wa reggae kutoka nchini Jamaica na Diamond ameweza kuwashirikisha katika ngoma yake inayokwenda kwa jina la Hallelujah.