Jinsi ya kupika halwa (halua)


Vipimo
Tambi za Mchele - Pakti 1 (400 mg)
Tui la nazi - Kikombe 1
Sukari - Nusu kikombe, ukipenda ongeza kidogo
Maziwa ya kopo (evaporated) - Nusu kikombe
Samli - Kijiko 1 cha supu
Zabibu kavu - ¼ Kikombe
Liki - ¼ kijiko cha chai
'Arki (rose flavour) - Matone matatu au zaidi
Namna Ya Kutayarisha Na Kupika

 1. Roweka majani ya chai vikombe 2 vya maji ya moto upate rangi iliyokoza.
 2. Chuja kwenye sufuria kubwa, mimina maji lita tatu na nusu au birika ya umeme mawili ya maji.
 3. Kwenye hayo maji tia, sukari, iliki,maji ya majani ya chai,zafarani na arki. Wacha mpaka ichemka.
 4. Wakati sufuria ipo jikoni chukua kibakuli utie unga wa conflour changanya na maji ya kawaida vikombe viwili.
 5. Mchanganyiko ukishakuaanza kuchemka mimina ule unga uliouchanganya na maji, koroga bila kuachia mkono kwa kutumia mwiko mrefu.
 6. Ukiona mchanganyika umeshashikana sawa sawa, mimina samli vikombe viwili.
 7. Endelea kukoroga bila ya kuachia na mchanganyiko ukiwamzito tia samli na endelea kukoroga. Muda wote koroga kwa mzunguko wa kuelekea upande mmoja tu kushoto au kulia. ( clockwise au anticlockwise)
 8. Utaendelea kufanya hivyo kwa masaa mawili mpaka mafuta yajitenge mbali na halua. Na yataanza kuruka ruka.
 9. Ili kujua kama halua tayari imeshawiva, ukiwa unakoroga chota kwenye kijiko kidogo uiache ipoe, kama inaonekana ipo ngumu baada ya kupoa , basi itakuwa tayari,la nilaini sana iwache kwenye moto huku unaendelea kukoroga mpaka iwe ngumu kwenye kijiko ikipoa.
 10. Ikiwa tayari tenganisha mafuta yote na halua.
 11. Baada ya hapo itie kwenye trays au vibakuli ya ufuniko na uipambie kwa kumwagia juu lozi zilizokatwa katwa.
Kidokezo:
Unaweza kupambia lozi , njugu au ufuta juu. Pia unaweka kwenye mchanganyiko vitu hivyo pale unakoroga ikiwa ipo jikoni.
Previous Post Next Post