Jinsi ya kupika tambi za mayai

Jinsi ya kupika tambi za mayai

Tambi za mayai ni moja kati ya vyakula ambavyo napenda kuandaa pale ninapokua nina haraka au sina muda mrefu wakukaa jikoni. Pishi hili huchukua muda mfupi sana na ni mlo uliokamilika.

Mahitaji


  • Tambi ½ paketi
  • Vitunguu maji 2 vikubwa
  • Karoti 1
  • Hoho 1
  • Vitunguu swaumu(kata vipande vidogo) kijiko 1 cha chakula
  • Carry powder kijiko 1 cha chai
  • Njegere zilizochemshwa ½ kikombe
  • Mafuta kwa kiasi upendacho
  • Mayai 2
  • Chumvi kwa ladha upendayo

Njia

1.Chemsha maji ya moto yanayotokota, ongeza chumvi na mafuta kidogo, weka tambi kwenye maji hayo chemsha adi ziive. Chuja maji yote ili kupata tambi kavu
2.Katika bakuli piga mayai kisha weka pembeni
3.Katika kikaango, weka mafuta, vitunguu maji, vitunguu swaumu, hoho, karoti na carry powder, kaanga kwa pamoja katika moto mdogo kwa muda mfupi kwani mboga hazitakiwi kuiva.
4.Ongeza tambi na njegere katika kikaango,geuza kila mara ili kuchanganya .
5.Ongeza mayai kwenye tambi kisha geuza kwa haraka bila kupumzika adi mayai yaive na tambi ziwe kavu.Tayari kwa kula

  • Katika hatua hii ongeza moto uwe wa wastani,moto ukiwa mdogo mayai yatafanya tambi zishikane na kufanya mabonge.

Unaweza kula tambi hizi na mboga yoyote upendayo au laa ukala zikiwa kavu na kufuraiha ladha yake zaidi.
Previous Post Next Post